siku chache
baada ya timu ya soka ya Pamba SC inayojiandaa na ushiriki wa ligi daraja la
kwanza msimu ujao kuichapa timu ya Mbao fc kwa jumla ya bao 1-0 katika mchezo
wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba wilayani Nyamagana
jijini hapa
Kocha mkuu wa timu ya Mbao FC Ettiene Ndayiragije raia wa Burundi
amesema kuwa timu ya Pamba inaweza kupanda daraja kwa uwezo waliooonyesha
katika mchezo huo.
Kocha
Ettiene Ndayiragije amesema kuwa wachezaji wa Pamba wanauwezo
mkubwa wa kuhakikisha kuwa timu hiyo inapanda daraja kurejea ligi kuu "
kwanza niwapongeze Pamba kwa ushindi na nimeona timu yao ina vijana wengi wenye
umri mdogo na wenye uwezo wa kupambana
hivyo ninaimani watafanya vizuri katika ligi daraja la kwanza msimu
ujao" alisema
Aidha
Ndayiragije amesisitiza kuwa licha ya Pamba kuwa timu bora kwa sasa wachezaji
nao wanatakiwa kushikana na kujituma wawapouwanjani " nimeambia hapa
Tanzania ligi daraja la kwanza huwa ni ngumu lakini kama hawa wachezaji wa
Pamba wakishikamana na kujituma kwa nguvu hakika Pamba inaweza kupanda daraja
na kurudi ligi kuu kwani timu yao ni nzuri na wanacheza vizuri" alisema
Mpaka sasa
timu ya soka ya Pamba imecheza jumla ya mechi 8 ambapo kati ya michezo miyo
imepoteza michezo mitatu ikishinda michezo 4 na kutoka sare mchezo mmoja.