Katika
kuhakikisha kuwa timu ya soka ya Stand United inafanya vema katika ligi kuu
tanzania bara timu hiyo imefanya mkutano mkuu wa mwaka ambapo pamoja na mambo
mengine mkutano huo ulijadili kwa kina mapato na matumizi ya timu hiyo ikiwa
sambamba na kupitisha bajeti mpya ya msimu wa mwaka 2017/18.
Kaimu katibu
mkuu wa timu hiyo Kennedy Nyangi amesema kuwa mkutano huo ulikuwa wa vuta
nikuvute kutokana na wanachama wa timu hiyo kuwa na shauku kwa timu yao kufanya
vizuri " mkutano wetu mkuu wa wanachama wa Stand United uliofanyika
septemba 3 mwaka huu ulienda vizuri na tumejadiliana vya kutosha na
tumekubaiana kwa pamoja kupitisha bajeti mpya ya msimu ujao" alisema
aidha Nyangi
amesisitiza kuwa moja ya vitu vilivyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na
jinsi ya kuboresha uendeshaji wa timu hiyo " kulikua na hoja ya kuboresha
uendeshaji wa timu yetu na tumekubaliana kwa pamoja kuhusu hilo na sasa kabla
ya msimu kuanza tutakuwa na bajeti yetu ambayo tumeiandaa sisi kaka kamati
tendaji na badae tutakua na mkutano mkuu kwaajili ya kuipitisha" alisema
Aidha Nyangi
aliongeza kuwa mkutano huo ulitumika kuwapatanisha baadhi ya viongozi wa timu
hiyo ambao walikuwa hawapatani " ni kweli kabisa katika timu yetu wapo
baadhi ya Viongozi walikuwa hawapatani na mkutano ule tuliutumia kuwapatanisha
kwani walikuwa wakilaumiana mara kwa mara lakini kwa sasa Viongozi wote wako
kitu kimoja na tutapambana kuhakikisha kuwa Stand United inafanya vema kattika
ligi" aisema