Siku
moja baada ya timu ya Toto African kutoka sare ya kutofungana na timu ya
Alliance sports academy katika mchezo wa nligi daraja la kwanza mchezo
uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini hapa aliyekuwa Kocha mkuu wa Toto African
Almas Mosh ametangaza kujiuzulu wadhifa wake katika timu hiyo.
Mosh
ameliambia championi kuwa sababu kubwa iliyopelekeaq yeye kubwaga manyanga
katika tiomu hiyo ni kutokana na timu yake aliyokuwa akiitumikia kushindwa kumlipa
nstahikizake “ Mim I nimeam,ua kujuzulku nafasi yangu ndani ya Toto African
kutokana na waajiuri wangu kusdhindwa kunilipa stahiki zangu jambo ambalo limenivunja moyo na kushindwa
kuendelea kuifundisha timu hiyo” alisema
Aidha
Mosh amesema kuwa tangu akabidhiwe mikoba ya kuifundisha timu hiyo tangu ishuke
daraja hajawahi kupewa maslahi yake hali iliyopelekea ajiuzulu kuifundisha timu
hiyo “ Mimi nimekabidhiwa mikoba ya kuiufundisha Toto African na usajili
nimefanya mwenyewe lakini mwisho wameshindwa kunilipa hata mshahara wangu hivyo
kuanzia leo mimi sio kocha wa Toto African “ alisema
Alipotafutwa mwenyekiti wa timu ya Toto African Godwin
Aiko ili kujibu taarifa hizo siku yake ya mkononi iliita bila kupokelewa na
alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya sms hakuweza kujibu ikumbukwe kuwa Kocha
Almas Mosh ameiongoza Toto African katika michezo miwili ambapo mchezo wa
kwanza timu hiyo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Biashara fc ya mkoani Mara
na mchezo wa pili timu hiyo ikatoka sare ya kutofungana na Alliance sports
academy hivyo mpaka sasa timu hiyo ina jumla ya pointi 1 katika michezo 2 iliyocheza.
Credit: Championi.