TOTO AFRICAN YALAZIMISHA SARE NA PAMBA SC

Oktoba 14, 2017
Wakati ligi daraja la kwanza ikiendelea kutimua vumbi timu ya soka ya Toto african imelazimisha kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Pamba sc zote kutoka jijini Mwanza, mchezo huo umeshuhudia wakazi wa Mwanza wakishuhudia burudani ya aina yake huku Pamba sc wakionyesha mchezo mzuri katika ligi hiyo iliyoendelea leo Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza licha ya kushindwa kuibuka na ushindi wa pointi 3 muhimu  baada ya mchezo wa hii leo Pamba imefikisha jumla ya pointi 3 baada ya michezo 5 hivyo bado iko nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi daraja la kwanza kundi C huku Timu ya Alliance schools ambayo itashuka dimbani kesho kumenyana na Transit Camp ikiwa na Pointi 10 kileleni. hata hivyo rekodi tangu timu hizi zikutane mchezo wa september 14 2013 Toto iliifunga Pamba bao 1-0 na marudio february 22 2014 Pamba nao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano  wa ligi daraja la kwanza. lakini mwaka 2016 Pamba ilifungwa na Toto bao 4-1 katika michuano ya kombe la FA na leo october 14 2017 timu hizi zimetoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Nyamagana.

last post see below

Next Article
« Prev Post
Previous Article
Next Post »
PEOPLE WHO COMMENT BELOW POST DROP YOUR OPINION
  • use this code to select difert type of word with bold use <strong></strong> or <b></b>.
  • for the italic use <em></em> or <i></i>.
  • To write letters underline use <u></u>.
  • To write letters strikethrought use <strike></strike>.
  • To write code HTML use <code></code> atau <pre></pre> atau <pre><code></code></pre>, And please put The code in the parser box below.

Disqus
OkUser Add your comment

Hakuna maoni