Octoba 14 mwaka huu Klabu ya Soka ya Pamba sc ilicheza na Toto
African mchezo wa Ligi daraja la kwanza kundi C na mchezo huo
kumalizika Kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja
wa Nyamagana jijini Mwanza.
Kabla ya mchezo huo kulikua na taarifa zikisambaa kwenye
mitandao ya kijamii kwamba kuna watu wasiojulikana wameingia katika
Uwanja wa nyasi bandia wa Nyamagana uliopo katikati ya Jiji la Mwanza
na kukata sehemu ya uwanja huo hali iliyopelekea uwanja huo kuwa na
sehemu yenye tundu katika uwanja huo ambapo badae Ofisa michezo wa Jiji
la Mwanza Mohamed Bitegeko ambaye pia ni Msimamizi wa Uwanja huo alithibitisha
kutokea Kwa tukio hilo na kusema kuwa hatua Kali zitachukuliwa Kwa
watakaobainika kuhusika na kitendo hicho cha kuukata uwanja wa Nyasi
bandia wa Nyamagana.
Sisi kama klabu ya Soka ya Pamba SC tunalaani vikali tukio
hilo kwakua siyo tukio la kiungwana Kwa Soka letu kwani Uwanja wa Nyasi
bandia wa Nyamagana umetumia muda zaidi ya miaka 2 kukamilika na
uwekezaji wa fedha nyingi umetumika hivyo tunalaani tukio hilo la
kukatwa Kwa sehemu ya Uwanja wa Nyamagana na tunaomba watakaobainika
wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho Kwa wengine hivyo Pamba
SC inalaani vikali kitendo hicho ambacho kimelidhalilisha Soka letu Kwa
kuamini imani za kishirikina kuliko maandalizi ya timu.
Lakini pia Klabu ya Pamba inakanusha vikali kuhusika na tukio hilo ambalo sio la kiuana michezo katika nchi yetu.
Lakini pia Klabu ya Pamba inakanusha vikali kuhusika na tukio hilo ambalo sio la kiuana michezo katika nchi yetu.
Picha chini inaonyesha sehemu ya Uwanja wa Nyamagana iliyokatwa