Na Mwandishi
wetu , Mwanza
Kwa sasa
ligi daraja la kwanza Tanzania bara iko katika mapumziko mafupi ya kupisha
dirisha dogo la usajili kwa timu za ligi daraja la pili, daraja la kwanza na
ligi kuu bara, wakati ligi hiyo ikiwa katika mapumziko timu ya soka ya Toto
African maarufu wanakishamapanda yenyewe iko mkiani mwa ligi hiyo kundi C ikiwa
na pointi 5 baada ya michezo 9 hali ambayo inawafanya wachambuzi wa maswala ya
soka kuitabiria timu hiyo huenda ikashuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza
kuelekea ligi daraja la pili kutokana na
mwenendo wake katika ligi hiyo ambapo yapo mengi ambayo yanachangia timu hiyo
kushindwa kufanya vizuri katika ligi hiyo na kujikuta ikitaka kutengeneza
rekodi ya kushuka daraja kutoka ligi kuu, daraja la kwanza na kisha ligi daraja
la pili.
VIONGOZI WABABISHAJI
Timu ya soka
ya Toto African kwa sasa iko chini ya wanachama wa Yanga wakiongozwa na
mtangazaji wa Radio free African Mtani Wambura ambao walidai kuwa timu toto ipo katika vipengele vya katiba ya Yanga
sasa najiuliza wanakuwaje viongozi wa Toto African wakati sio wanachama wake ?
na pia kazi zake za uandishi wa habari na utangazaji zimemshinda? Hakika huu ni
ubabaishaji mwingine unaopelekea timu hiyo kuvurunda katika timu hiyo lakini
pia hawa yawezekana wametumwa kuisambaratisha timu ya wanakisha mapanda.
KUPOTEZA
MECHI KIZEMBE
Wakati ligi
daraja la kwanza kundi C ambayo Toto African inashiriki ikiendelea kuliibuka
mingong’ono miongoni mwa wadau wa soka jijini Mwanza kuwa Toto African wameanza kujihusisha na
maswala ya kuuza mechi jambo ambalo halijathibitishwa na yeyote mpaka sasa
hivyo kama ni kweli hilo nalo linaweza kusababisha timu hiyo kushindwa
kuonyesha ushindani wowote katika ligi hiyo kwani yawezekana wachezaji hawapati
stahiki zao na kupelekea kutijituma wawapo Uwanjani na tetesi za viashiriavya
kuuza mechi vilianzia mechi ya Toto African na Biashara toto akifungwa bao 3-1 na kisha mechi ya Toto
African na Alliance schools ambapo Toto walifungwa bao 4-1.
WACHEZAJI
KUTENGWA
Baada ya
ligi daraja la kwanza kumalizika kwa mzunguko wa 9 wa ligi hiyo huku timu
zikiwa katika mapumziko mafupi na
harakati za kufanya usajili wa dirisha dogo baadhi ya wachezaji wa Toto
African ambao waliletwa na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Timu hiyo Wazir Gao
kutoka jijini Dar es salaam waligomewa kuhudumiwa huku baadhi ya Viongozi wa
Toto wakisema kuwa wachezaji hao waondoke katika timu hiyo kitu ambacho kinaua
ukuaji wa soka letu na ustawi wa Toto African kwa ujumla na mpaka sasa
wachezaji hao wasiozidi watatu tayari wamesafirishwa kurejea jijini Dar es
salaam .
MWENENDO
WAKE KATIKA LIGI HIYO
Toto African
imekuwa na mwendendo ambao sio mzuri hivyo lazima Uongozi wa juu wa timu hiyo
Chini ya mwenyekiti wa timu hiyo Godwin Aiko lazima wajipange upya kuhakikisha
kuwa wanaisaidia timu hiyo kufanya vema katika ligi hiyo kwani katika kundi C
endapo Toto African wakijiandaa na kufanya usajili katika dirisha dogo wanaweza
kujikwamua na kufanya vema lakini endapo wataendeleza mizaha hakika safari ya kushuka
daraja itawadia kwao.
MWENYEKITI
AITISHA MKUTANO WANACHAMA WAUGOMEA
Novemba 19
mwaka huu mwenyekiti wa timu ya Toto
African Godwin Aiko aliitisha mkutano mkuu wa dharula kwa timu hiyo huku ajenda
ikiwa ni kujadili mwenendo wa timu hiyo katika ligi daraja la kwanza ambapo
mkutano huo ungefanyika kwenye ukumbi wa bwalo jijini hapa lakini cha ajabu
wanachama wa timu hiyo waligoma kujitokeza katika mkutano huo hali ambayo
imeendelea kupoteza matumaini ya ushiriki wao katika ligi daraja la kwanza
msimu huu lakini siku mbili baadae mkutano ulifanyika na wakaazimia kwa nguvu
moja kuungana na kuwa kitu kimoja ili timu hiyo iweze kunusurika kushuka daraja.
USHAURI KWAO
Kutokana na
ligi daraja la kwanza kuwa ngumu basi timu hiyo ijipange upya isiweze kushuka
daraja kwani ikishuka daraja hakika haitaonekana tena katika medali ya soka.