Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mwanza Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Nyanza Bottling Company Limited kwa mikoa ya kanda ya ziwa Samwel Makenge amesema kuwa wameamua kuja na ofa hizo kwa wakazi wa kanda ya ziwa ili kuongeza msisimko kuelekea kombe la Dunia " sisi kama Kampuni ya Cocacola tumeamua kuwajali wateja wetu ambapo tumeamua kuja na Promosheni ya Cocacola na mzuka wa soka ambapo katika ofa hii wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa watanufaika na ofa hii kwa kununua soda za Cocacola, Fanta aina zote, Sprite na Stone Tangawizi ambapo wataweza kujishindia TV Flat screen, Soda za bure, Pesa taslimu pamoja na Bodaboda" alisema
Makenge ameongeza kuwa baada ya mteja kununua soda ya cocacola na atafunua kizibo kama akikuta ameshinda ataweza kupata zawadi katika maeneo yafuatayo " kama Mteja wetu akinunua soda na kukuta ameshinda zawadi, zawadi zetu zitatatolewa katika maeneo mbalimbali kwanza kama mteja akishinda zawadi ya soda za bure atapewa zawadi yake dukani aliponunua soda au kwenye gari letu la mauzo, kwa wale watakaoshinda fedha watajipatia fedha Kiwandani au kwa mawakala wetu lakini pia hata kwenye vituo vyetu vilivyoidhinishwa na kampuni yetu, na wale watakaoshinda TV na Pikipiki watapata zawadi zao kiwandani pia na fedha taslimu zitakazotolewa ni kuanzia shilingi 5000, 10000, pamoja na laki moja kwa ujumla fedha ambazo zimetengwa kama zawadi ni shilingi milioni 800" alisema
Makenge amewaomba wakazi wa Kanda ya ziwa kununua vinywaji vya kampuni ya coca-cola kwani wanaweza kujipatia zawadi zilizotajwa " nichukue fursa hii kuwaomba wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kuchangamkia fursa hii kwani wataweza kujipatia zawadi mbalimbali ikiwemo TV ambazo watazitumia kulitazama kombe la Dunia lenyewe kwani tumefanya hivi kwakua sisi Cocacola ndio wadhamini wa kuu wa kombe la Dunia.