mchezo huo umechezwa tofauti na ulivyotegemewa ambapo waamuzi katika mchezo huo wamechezesha kwa kiwango cha hali ya juu lakini pia matokeo hayo yanaiweka timu ya Toto african katika hali mbaya zaidi ya kushuka daraja ambapo mpaka sasa imcheza jumla ya michezo 11 na kufanikiwa kujikusanyia pointi 6 pekee .
Matokeo katika ligi hiyo timu ya Biashara fc ya Musoma mkoani Mara imeichakaza timu ya Alliance kwa bao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Karume Mara huku Dodoma fc wao wakifungwa bao 2-0 na Rinho Rangers mchezo uliopigwa Uwanja wa Alhasan mwinyi Tabora.