Klabu ya soka ya Pamba Sc inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara inatarajia kuwa na Mkutano wake utakaofanyika Mei 20 mwaka huu kuanzia majira ya saa 9:00 Alasiri ambapo utafanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Aden Palace iliyoko wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Lengo kuu la Mkutano huo ni kujadili mwenendo na Maandalizi kuelekea ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao ambapo wahusika katika mkutano huo ni pamoja na Wachezaji wa Zamani wa Pamba Sc, Wadau, wapenzi na mashabiki wa timu ya Pamba ambayo imekuwa na historia kubwa katika soka la Nchi yetu.
Mnaombwa kufika bila kukosa katika mkutano huo ambao ndio utakaotoa Mustakabali wa timu yetu kushiriki ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao na hatimaye kupanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara.