Na Mwandishi wetu Shinyanga
Aliyekuwa Shabiki wa timu ya Yanga Ally Mohamed maarufu kama Ally Yanga leo amezikwa katika makaburi ya Nguzo nane mkoani Shinyanga baada ya kufariki akiwa katika msafara wa Mbio za mwenge wa Uhuru wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma akizungumza na Mwanzasports house Hashim Omary ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga amesema kuwa mazishi hayo tayari yamefanyiika " Nikweli sisi kama mashabiki wa Yanga mwanza tumeungana na wenzetu huku Shinyanga kwaajili ya kumsitiri mwenzetu na amezikwa makaburi ya Nguzo nane" alisema
Marehemu Ally Yanga alikuwa mhamasishaji mkubwa ndani ya timu ya Yanga pamoja na timu ya Taifa ambapo Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania DR John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa baada ya kuondokewa na mpendwa wao