Klabu ya soka ya Simba SC ya jijini Dar es salaam leo imemsajili Mlinzi wa kati na kiungo, Yusuph Mlipili kwa Mkataba wa Miaka mitatu (3).
Pichani Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kuburu' (kushoto) akimsainisha kandarasi Mlipili ambaye msimu uliopita aliichezea Toto Africans ya Mwanza iliyoshuka daraja.
Ikumbukwe kuwa mpaka sasa wachezaji Yusuph Mlipili , Salum Chuku na Wazir Junior wote walikuwa wakiichezea Toto African msimu uliomalizika na sasa wanakula maisha baada ya timu yao kushuka daraja, Wazir Junio amejiunga na Azam fc, Salum Chuku amejiunga na Singida United huku Yusuph Mlipili akijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo kwa dili ambalo halijawekwa wazi.