Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Kulia akiwa ameshika mpira wa kikapu akizundua mashindano ya Umiseta kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela.
Na Janeth James,Mwanza
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan leo juni 8 ameyazindua rasmi mashindano ya shule za sekondari taifa( Umiseta) kwenye uwanja wa CCM Kirumba mashindano ambayo yatakuwa yakifanyika kwenye viwanja vya Chuo cha ualimu kilichopo Butimba wilayani Nyamagana jijini hapa kwa mara ya 38 tangu kuanzishwa kwake huku yakifanyika kwa mara ya pili mfululizo jijini Mwanza,, Katika uzinduzi wake Mama Samia amewaomba wanafunzi kuhakikisha kuwa wanalinda na kuendeleza vipaji vyao ili akina Mbwana Samatta wapatikane wengi " nawaomba sana wasimamizi wa mashindano haya muhakikishe kuwa mnalea na kukuza vipaji vya watoto hawa kwani ni aibu kwa nchi yetu kila mwaka kushindwa kufanya vema katika mashindano ya kimataifa" alisema