Na Mwandishi wetu Nyamagana
Wakati ligi daraja la nne ngazi ya wilaya ya Nyamagana ikiendelea kutimua vumbi timu ya Iseni fc kutoka wilayani Nyamagana imeichapa bila huruma timu ya Buhongwa fc kwa jumla ya bao 6-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Nyamagana uliopo katikati ya jiji la Mwanza hata hivyo timu ya Iseni fc imekuwa timu ya pili kufunga mabao mengi katika ligi hiyo baada ya timu ya Nyamwaga fc kushinda bao 9-0 dhidi y Mlango mmoja fc.