Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Chile na timu ya Arsenal ya nchini England Alex Sanches ambaye kwa sasa yuko kwenye majukumu ya kuitumikia timu yake ya Taifa amesema kuw ampaka sasa hajajua msimu ujao atachezea timu gani licha ya kubakiza mwaka mmoja kwenye kkataba wake na timu ya Arsenal.
Sanchez mwenye umri wa miaka 28 amesema kuwa timu anayoipenda ni Mancester City ila kutokana na yeye kuwa na mkataba na Arsenal hajui ataenda wapi " Mimi naipenda sana Manchester City ila bado nina mkataba na Arsenal hivyo sijui nitakuwa wapi msimu ujao" alisema
na alipoulizwa kama anapenda kucheza na kipa wa timu yake ya Taifa Claudio Bravo amesema " kwa sasa siwezi kulijibu hilo ila ngoja tumalize fainali ya kombe la mabara nitaamua wapi pa kwenda"
kwa msimamo huo huenda Sanchez akajiunga na Manchester City akitokea Arsenal na kuungana na kipa Claudio Bravo ambaye ameibuka shukaa katika timu yake ya Taifa kwa kuokoa penati tatu na kuiwezesha Chie kucheza Fainali ya kombe la Mabara na Ujerumani.