Na wandishi wetu
Wenyeji wa michuano ya FIFA Confederation Cup timu ya taifa ya Rasia imefanikiwa kuyaanza vema mashindano hayo baada ya kuichapa timu ya New Zealand kwa bao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sant Petersburg nchini Rasia, katika mchezo huo ulishuhudia Raisi wa nchini hiyo Vladimir Putin akiwaongoza wananchi wake kuishangilia timu yao na kufanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo wa ufunguzi,
Wachezaji wa timu ya taifa ya Urusi wakichangilia bao katika mchezo huo
Urusi ambao wako kundi A wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi 3 huku kesho mchezo wa Mexico na Ureno ukitarajia kupigwa ili kupata uwiano sahihi wa kundi hilo ikumbukwe kuwa Bingwa wa michuano hiyo ya FIFA Confederation Cup atajipatia kitita cha fedha za kitanzania bilioni 11.