Klabu ya Singida United ya mkoani Singida iliyopanda daraja kucheza ligi kuu bara msimu ujao imemsajili kwa mkataba wa miaka miwili (2), Mshambuliaji Danny Usengimana kutoka Polisi Rwanda.
Nyota huyo anayeichezea timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' ametambulishwa rasmi.
Usenginimana amekuwa mfungaji bora misimu miwili mfululizo katika Ligi kuu ya Azam Rwanda Premier League
Singida United ambayo kwa sasa iko chini ya Kocha wa zamani wa Yanga Hans Van Der Pluijm imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa ligi baada ya kusajiri nyota kadhaa ambao kwa hakika wataisaidia timu hiyo kufanya vema katika ligi kuu msimu ujao..