Na Janeth James, Singida
Msanii wa nyimbo za injili hapa nchini, Rose Mhando anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida kwa mahojiano kufuatia tuhuma zinazomkabili za kijipatia sh. 950,000 kwa njia ya udanganyifu, Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba amesema msanii huyo aliweka chini ya ulinzi Juni Mosi mwaka huu majira ya mchana wilayani Ikungi baada ya waumini wa kanisa la AICT Singida kupata taarifa msanii huyo hupo wilayani humo.
Kamanda Magiligimba ameeleza mnamo November 3 mwaka jana majira ya saa nne asubuhi stendi ya mabasi Misuna, Mwenyekiti wa kaya ya AICT Singida, Mashara Japhet alimtumia Rose Mhando (38) Mzigua mkazi wa Ipagara Dodoma fedha Sh. 800,000 kwa njia ya M-Pesa kwa makubaliano angeweza kufika kwenye uzinduzi wa kwaya ambao ulipangwa kufanyika November 8 mwaka jana lakini hakufanya hivyo.
Aliongeza kabla ya kufika siku ya uzinduzi Rose Mhando aliomba kutumiwa Sh. 150,000 kwa ajili ya nauli ya kuwasafirisha kutoka Dodoma kwenda Singida akiwa na wasaidizi wake lakini hata alipotumia hakufika na siku ya uzinduzi wakapata taarifa msanii huyo yupo Kahama mkoani Shinyanga akifanya huduma, na ilipofika Juni Mosi mwaka huu ndipo walipata taarifa msanii huyo yupo mkoani humo ndipo walipofuatilia na kumkamata.
CREDIT: BONGO 5