Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Simba Ibrahim Ajibu leo amesaini mkataba wa kuichezea timu ya Simba kwa muda wa miaka miwili na kukabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa ikivalia na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Jerson Tegete ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Mwadui fc ya Shinyanga,
Ajib anajiunga na Yanga baada ya mkataba wake na timu ya Simba kufika ukingoni juni 30 mwaka huu, kutokana na hali ilivyo Ajibu ni moja ya wachezaji wenye vipaji vikubwa hapa nchini na huenda akaisaidia sana timu yake ya Yanga katika michezo ya kimataifa.
Ikumbukwe kuwa mapema mwezi February mwaka huu Ibrahim Ajib aliifunga Yanga bao katika ushindi wa bao 2-1 ambapo katika mchezo huo Simba walipewa kadi nyekundu ya Besela Bokungu na Simba kushinda bao 2-1 dhidi ya Yanga.