Klabu ya soka ya Singida United Fc ya mkoani Singida leo imemsajiri aliyekuwa Winga wa kulia wa Stand United na Simba Sport Club, Pastory Athanas kwa kandarasi ya miaka miwili.
Pastory Athanas ni moja ya wachezaji wazuri kutokea mkoani Simiyu lakini hakuwa chaguo kwa kocha Omog wa Simba, hivyo ameamua kupeleka huduma yake kwa timu ya Singida United Fc.
Hapo pichani ni Pastory Athans akikabidhiwa jezi na Mkurugenzi wa Singida United ndg.Festo Sanga
Ikumbukwe Pastori alijiunga na timu ya Simba mwezi desemba mwaka jana katika usajiri wa dirisha dogo laini amekuwa hapewi nafasi ndani ya kikosi cha wekundu wa msimbazi.