Na Mwandishi wetu Mwanza
Timu za Singida United ya mkoani Singida na timu ya Alliance sports academy ya Mwanza zinatarajia kukutana kwa mara ya kwanza tangu Singida United wapande daraja kucheza ligi kuu, timu hizo zitakutana katikamchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza july 22 mwaka huu.
Alliance kwa sasa inafanya maandalizi yake ya kujifua kuelekea ligi daraja la kwanza huku Singida United wao wakijiweinda na ushiriki wa ligi kuu bara msimu ujao. Ikumbukwe kuwa mwaka huu mwezi February tmu hizo zilikutana na Singida ikaifunga Alliance kwa bao 3-1 na kupanda daraja hivyo huenda mchezo huo ukawa wa kulipa kisasi kwa timu hizo mbili.