baada ya
timu ya Singida United kupanda daraja kucheza ligi kuu bara huku timu ya
Alliance sports academy ikiendelea kusota ligi daraja la kwanza timu hizo
zinatarajia kukutana kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa
jumamosi hii kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa baada ya timu ya Singida
united kuichapa Alliance kwa bao 2-0 na kupanda ligi kuu bara mwezi february
mwaka huu.
kwa upande
wa waandaji wa mchezo huo ambao ni chama cha soka wilaya ya Nyamagana NDFA kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya
mashindano ya chama hicho Suleiman Kiggi amesema kuwa lengo la kuandaa mchezo
huo ni kutoa burudani kwa wakazi wa
Mwanza " sisi kama Nyamagana tumeamua kuandaa mchezo huu ili mashabiki wa
soka Mwanza waweze kupata burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu baina ya
timu hizo mbili " alisema
Naye Ofisa
habari wa timu ya Alliance sports academy Jack Mwafulango amesema kuwa timu
yake iko tayari kucheza mchezo huo wa majaribio kuelekea ligi daraja la kwanza
" timu yetu ya Alliance tayari imeanza maandalizi kushriki ligi daraja la
kwanza hivyo sisi tutaucheza mchezo huo na ikiwezekana tutalipa kisasi kwa timu
hiyo ambayo ilitufunga mabao 2-0 kwao na kuoanda ligi kuu" alisema
Aidha Mwenyekiti
wa kamati ya mashindano ya chama cha soka wilaya ya Nyamagana Suleiman Kiggi
amewaomba wadau wa mchezo wa soka kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo
unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 10 jioni " tunawaomba wadua na
mashabiki wa timu hizi mbili wajitokeze kwa wingi kesho jumamosi ili waweze
kushuhudia mtanange huo ambao naamini utakuwa na ushindani wa aina yake"
alisema
Chanzo: Championi.