Kocha mkuu
wa Mbao fc Ettiene Ndayiragije amesema kuwa wiki hii ndiyo wiki ya mwisho kwa
wachezaji ambao wanahitaji kufanya majaribio ya soka la kulipwa kwa timu hiyo
na kuanzia wiki ijayo ataanza programu nyingine ikiwemo kucheza michezo mingi
ya kirafiki kuelekea ligi kuu Bara.
Akizungumza
na Championi Koocha Ndayiragije amesema kuwa licha ya kujitokeza wachezaji
wengi lakini amefanikiwa kupata wachezaji wazuri " sisi tumeanza kuchagua
wachezaji kwenye kliniki yetu kwa zaidi ya wiki tatu na tangu tulipoanza
tulipata wachezaji zaidi ya 200 ambao walihitaji kufanyiwa majaribio na tayari tumepata wachezaji ambao
tutawatumia katika ligi ya msimu ujao " alisema
Aidha
Ndayiragije amesema kuwa mwisho wa kufanya mchujo kwa wachezaji ni jumapili hii
ambapo baada ya hapo Mbao itaanza maandalizi yake rasmi "kama
kunawachezaji ambao bado wanahitaji kufanyiwa majaribio ya soka katika timu
yetu wanatakiwa kufika kabla ya siku hizo ili waweze kufanyiwa majaribio kama
wakitufaa tutawachukua kwani tunahitaji kuwa na kikosi kipana sana ambacho
kitaisadia Mbao kufanya vema katika michezo yake kwenye ligi" alisema
Mbao fc
inajiandaa kushiriki ligi kuu Tanzania bara huku timu hiyo ikiwa imefanya
mabadiriko ya viongozi wake ambapo Kocha msaidizi kwa sasa ni Hamad Ally, huku
Katibu mkuu akiwa Daniel Naila ambaye ni mhadhiri wa chuo cha mtakatifu
agustino (SAUT) jijini hapa.