Katika
kuhakikisha kuwa timu ya Pamba inapanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara
msimu ujao timu hiyo imemsajili aliyekuwa beki wa kati wa timu ya Alliance sports academy Juma Nyangi kwa
mkataba wa mwaka mmoja kwaajli ya kuitumikia
timu hiyo ambayo inajiandaa kushiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Akizungumza
na Championi Mtendaji mkuu wa timu ya Pamba Bob Butambala amesema kuwa wao kama
timu wamefuata taratibu zote zinazotakiwa kumnasa mchezaji huyo " Kwakua
tunataka kupanda daraja kucheza ligi kuu sisi tumefuata taratibu zote
kuhakikisha kuwa tunapata wachezaji wazuri akiwemo Juma Nyangi hivyo lengo la
Pamba kwa sasa ni kupanda daraja kucheza ligi kuu baada ya kushindwa kufanya hivyo
miaka mingi" alisema
Aidha
Butambala ameongeza kuwa Juma Nyangi amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia
timu hiyo ambayo yatari imeanza mikakati yake " Pamba fc ni kweli
imemsajiri mchezaji Juma Nyangi anayemudu kucheza nafasi ya beki wa kati kwa mkataba
wa mwaka mmoja akitokea Alliance na sisi tumefuata taratibu zote hivyo
tunaendelea kujipanga ili Pamba fc irejee ligi kuu bara kuleta ushindani kama
ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma" alisema
Butambala
amesisitiza kuwa Pamba fc inatarajia kuanza kambi yake julai 22 mwaka huu lengo
ikiwa ni kuanza maandalizi ya ligi daraja la kwanza " timu inatarajia
kuanza kambi yake julai 22 na lengo la kufanya hivyo ni kuajiandaa na ushiriki
wa ligi daraja la kwanza ambayo haina wadhamini na sisi kama Pamba kwa kauli moja
tumedhamiria kuipandisha ligi kuu timu yetu " alisema
Chanzo: Championi.