Na Mwandishi wetu, Madrid
aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Real Madrid Alvaro Morata amewaaga wachezaji wenzake na tayari kujiunga na Chelsea ambao wamelipa paun milioni 70 na tayari Morata amekubaliana na Chelsea kuhusu maslahi yake ndani ya klabu hiyo, Ikumbukwe kuwa ni kama Chelsea wamelipiza kisasi kwa Manchester United ambao hapo awali Chelsea walijiandaa kumsajiri Rumelu Lukaku lakini Manchester wakamuwahi mchezaji huyo na kuipiga chapuo Chelsea na The Blues wamemsajiri Alvaro Morata na kujisuuza roho baada ya kukwapuliwa Lukaku.