Kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF, imemfungulia wakili Damas Ndumbaro aliyefungiwa na shirikisho hilo kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka saba sambamba na kocha msaidizi wa Geita Gold, Choki Abeid baada ya kubaini kuwa hoja zilizotumika kuwafungia hazikuwa na mashiko.
Wakati huohuo aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha soka Tabora (Tarefa), Yusuph Kitumbo, na katibu wake Fethi Remtullah pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa timu ya JKT Oljoro, Thomas Mwita, adhabu zao zitaendelea kama kawaida