Waziri wa
Mambo ya nchi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba magharibi mkoani Singida Mwigulu Nchemba ameitabilia
vema timu ya Alliance sports academy ya jijini hapa kuwa huenda timu hiyo
ikapanda daraja msimu ujao kutokana na uwezo waliouonyesha Uwanjani katika
mchezo wa kirafiki na Singida United ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Singida
United kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Akizungumza
na mtandao huu mara baada ya mchezo huo kumalizika Waziri Mwigulu amesema kuwa
alliance ni timu nzuri kwani licha ya Singida United kushinda mchezo huo wa
kirafiki lakini mchezo ulikuwa mgumu sana " Mimi nimeona jinsi ambavyo
Alliance waoanyesha ushindani katika michezo yao hiyo kuna uwezekano mkubwa kabisa
timu hii ikapanda daraja" alisema
Aidha
Nchemba aliongeza kuwa sababu kubwa iiyoifanya Alliance ishindwe kupanda daraja
msimu uliomalizika ni kwakua ilitakiwa timu moja tu " Msimu uliopita wa
ligi daraja la kwanza ulikuwa mgumu sana kwani Singida walijiandaa kupanda na
Alliance pia walijiandaa kupanda hivyo katika michezo yao Alliance sports
acadey alipoteza mchezo wake dhidi ya Singida na Singida akapoteza mchezo dhidi
ya Alliance hali hiyo ilionyesha dhahiri kwamba timu zote zilikuwa na
maandalizi na Singida waliuwa na bahati ya kupanda ligi kuu" alisema
Katika hatua
nyingine Mwigulu amewashukuru wadau wa michezo katika jiji la Mwanza kwa jinsi
wanavyozipenda timu zao na kuwaasa kuendelea kuziunga mkono timu zao "
kiukweli mnanitia moyo sana kuona mnajitokeza kusisapoti timu zenu hivyo
nawaombeni muendelee kuiunga mkono Alliance itapanda daraja msimu ujao kwani
mipango na nia wanayo" alisema