Katika hali
iliyowashangaza wengi ni pale wachezaji watatu wa familia moja ambao ni Kiggi
Makasi, Geofrey Makasi pamoja na Martine Kiggi kucheza Uwanja mmoja katika
mchezo wa kirafiki ambapo Alliance sports academy walifungwa na Singida United
kwa bao 2-0 mchezo uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini hapa.
katika
mchezo huo uliokuwa na upinzani wa aina yake ulishuhudia Kiggi Makasi ambaye
anaichezea timu ya Singida United akiwaadabisha wadogo zake ambao wanaichezea
Aliance ambapo pamoja na mambo mengine alisababisha penati ambayo ilizaa bao la
pili.
Baba Mzazi
wa wachezaji hao Luseke Kiggi amesema kuwa anajivunia sana kuona watoto wake
wanacheza soka katika Uwanja mmoja " ni nadra sana kuona wachezaji
wanaotoka familia moja wakicheza Uwanja mmoja hivyo mimi nafurahi sana kwani
familia yetu ni familia ya mpira kwani hapo kabla mimi mwenyewe niliwahi
kucheza soka katia timu za Pamba na nyingine hivyo najivunia kuona wtoto wangu
wakicheza soka katika Uwanja mmoja" alisema
kwa upande
wake Kiggi Makasi ambaye alikuwa akiichezea Ndanda kabla ya kujiunga na Singida
United amesema kuwa hata yeye amefurahi sana kuona anacheza Uwanja mmoja na
wadogo zake " Nimefurahi sana kuona nacheza na wadogo zangu na nimeona
wanacheza vizuri na wakiongeza juhudi watafika mbali zaidi hivyo nimefurahi
sana " alisema
Ikumbukwe
kuwa Martine Kiggi pamoja na Geofrey Kiggi wanaichezea Alliance sports academy
na walikutana na kaka yao Kiggi makasi anayeichezea Singida United na Singida
kufanikiwa kuifunga Alliance kwa bao 2-0.