Timu ya soka
ya Alliance sports academy inayojiandaa na ushiriki wa ligi daraja la kwanza
msimu ujao imelazimisha sare ya kutofungana na timu ngumu ya Kagera Sugar
katika mchezo wa kirfaiki uiopigwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambapo Kagera
Sugar waliutumia mchezo huo kuwatangaza wachezaji wao wapya.
Kocha mkuu
wa Alliance sports academy Mbwana Makata alisema kuwa mchezo huo ulikuwa na
ushindani mkubwa kwa timu zote kwani kila timu ilicheza kwa uwezo wake "
katika mchezo wetu na Kagera Sugar tuliona kuna ushindani mkubwa na tumepata
kipimo tosha kuelekea ligi daraja la kwanza msimu ujao kwani Aliance inahitaji
kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao" alisema
Aidha Makata
amesisitiza kuwa mchezo huo umempa mwanga na baadhi ya makosa ambayo bado
yanajitokeza " mara baada ya kumalizika kwa mchezo wetu nilibaini kuwa
timu yetu bado inamapugufu makubwa hasa upande wa ushambuliaji hivyo
nitayafanyia kazi eneo hilo ili timu yetu iwe inapata matokeo katika michezo
yake ya ligi daraja la kwanza" alisema
Kwa upande
wake Kocha mkuu wa Kagra Sugar Meck Mexime amesema kuwa mchezo wa timu yake
dhidi ya Alliance umekuwa kipimo izuri kwa wachezaji wake kabla ya ligi kuanza
na ameahidi kuisuka Kagera kuwa timu bora ya kiushindani " mchezo wetu na
Alliance ni mchezo mzuri na umewapima wachezaji wangu vya kutosha hvyo nawaomba
mashabiki wa timu yetu waendelee kutuunga mkono" alisema