wakati mkoa
wa Mwanza ukiwa na jumla ya timu 3 zinazojiandaa na ushiriki wa ligi kuu bara
na ligi daraja la kwanza mkuu wa mkoa wa
Mwanza John Mongella amesema kuwa hawataisapoti timu yoyote itakayokuwa na
viashiria vya kuuza mechi au kucheza michezo yao chini ya kiwango kwa makusudi.
Mkuu huyo wa
mkoa wa Mwanza ameyasema hayo wakati akizindua kipindi cha tujadiliane kipindi
ambacho kimeanzishwa na Umoja wa waandishi wa habari Tanzania ambapo amesema
kuwa mkoa wa Mwanza uko tayari kuzisaidia timu za Mwanza ambazo zitaonyesha
jitihada " sisi kama mkoa tutazisaidia zile timu ambazo zitaonyesha juhudi
lakini timu yoyote itakayocheza chini ya kiwango katika ligi kuu au daraja la
kwanza hatutahangaika nayo" alisema
aidha
Mongella amesisitiza kuwa kumekuwa na utamaduni wa serikali ya mkoa kuzisaidia
timu kupata udhamini lakini wanashindwa kuutumia vizuri " mkoa wa Mwanza
tunatamani tuwe na timu zaidi ya moja ligi kuu lakini timu zingine zinakuwa na
viashiria vya kuuza mechi na zingine hucheza chini ya kiwango ila tmejipanga
kuzisaidia zile timu ambazo zinaonyesja juhudi" alisema
Mongella
amesisitiza kuwa mwaka huu atahakikisha kuwa anashirikiana na timu za Toto
african , Pamba na Alliance ii timu moja ipande daraja kucheza ligi kuu msimu
ujao " kama mkoa tutahakikisha kuwa timu moja inapanda daraja kucheza ligi
kuu msimu ujao ili mkoa uwe na timu mbili ligi kuu na tutaanza kuziangalia timu
itakayoonyesha nidhamu tutaitafutia ufadhili" amesema.