Aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho la soka nchini #Tanzania,#WallaceKaria amechaguliwa kuwa Rais mpya wa shirikisho la kabumbu nchini Tanzania-TFF baada ya kupata kura 95 kati ya 128 zilizopigwa na wajumbe huko mkoani #Dodoma.
Aliyefuata ni #Ali Mayay aliyepata kura 9 sambamba na Shija Richard kura 9,kati ya kura 128 kura mbili ziliharibika.
#Michael Wambura amechaguliwa kuwa makamu wa Rais kwa kupata kura 85 kati ya 128 zilizopigwa huku mpinzani wake wa karibu akipata kura 25 ambaye ni #Mulamu Ng'ambi.
Katika nafasi ya makamu wa Rais kura 3 ziliharibika.