Chama cha
soka wilaya ya Nyamagana NDFA kimekilaumu chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA
kwa kusitisha mashindano ya ligi ndogo kwaajili ya timu 4 za Mwanza ambayo
yalipangwa kufanyika tangu agosti 7 mwaka huu kwa lengo la kuzisaidia timu
kujua mapungufu ya timu zao.
Katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Nyamagana Dady Gilbert
alisema kuwa wao kama chama waliamua kuandaa ligi hiyo ili timu zijue mapungufu
ya timu zao kabla ya ligi kuuu na ligi daraja la kwanza " sisi kama chama tuliamua kuanzisha ligi
ndogo kwa kushirikisha timu 4 za ligi kuu na ligi daraja la kwanza lakini
chakushangaza Katibu wa chama cha soka mkoa Leonarl Malongo amekuja juu na
kututaka tusitishe mara moja lii hiyo kitu ambacho ni kudumaza soka katika mkoa
wetu" alisema
aidha Dady
alisisitiza kuwa kwakua chama cha soka mkoa hakina maono ndiyo maana wao
waliamua kuanzisha ligi ndogo kwa faida ya timu za Mwanza zinazokwenda
kushiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza " sisi baada ya kuona Chama
cha soka mkoa wako kimya tukaamua kuanzisha ligi hii ambayo ingeshirikisha timu
za Toto african, Pamba fc , Mbao fc pamoja na Alliance lakini katibu amekuja na
kutuzuia hivyo wadau watambue kwamba hao ndio viongzi waliowachagua ambao
hawataki soka liendelezwe kwa misingi yote" alisema
alipotafutwa
Katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa Mwanza mzfa Leonard Malongo kuzungumzia sakata hilo
simu yake haikupatikana mpaka gazeti linakenda mitamboni simu yake ya mkononi
haikupatikana kabisa.