Aliyekuwa
kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga ambaye kwa sasa anakipiga katika timu ya
Mbeya City Mrisho Ngassa ameonekana akifanya mazoezi ya kujiweka fiti kuelekea
ligi kuu msimu ujao akiwa na Pamba fc katika mazoezi yake yanayoendelea mkabala
na Uwanja wa ndege wa jijini Mwanza.
Ngassa
ambaye ni mchezaji wa zamani wa Free states ya nchini Afrika kusini ameonekana
akifanya mazoezi na timu ya Pamba ambapo baadhi ya mazoezi aliyofanya ni pamoja
na kukimbia, kunyoosha Viungo pamoja na kucheza mchezo ambao ulidumu kwa dakika
75.
Ngassa
ameliambia Championi kuwa lengo la kufanya mazoezni na Pamba sio kwamba
amesajiliwa na Pamba bali anauweka fiti mwili wake kuelekea ligi kuu bara msimu
ujao " Kimsingi nilikuja Mwanza kwa matatizo ya kifamilia na nikaona ni
vyema nifanye mazoezi na Pamba fc na lengo la kufanya hivyo ni kuweka mwili
wangu kuwa katika hali nzuri ili niisaidie timu yangu ya Mbeya City iweze
kufanya vizuri katika ligi ya msimu ujao" alisema
Ikumbukwe
kuwa Pamba fc kwa sasa inajiandaa na ligi daraja la kwanza ambapo tayari
imeanza mazoezi yake na matarajio yake
ni kuhakikisha kuwa timu hiyo inapanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao ndiyo
maana Mrisho Ngassa amesema kuwa amwvutiwa na maandalizi ya timu hiyo "
Nimevutiwa sana na maandalizi ya Pamba nina imani watafanya vizuri zaidi
kuelekea ligi daraja la kwanza" alisema