wakati ligi
daraja la nne ngazi ya wilaya ya Nyamagana ikiendelea kutimua vumbi katika
Uwanja wa Nyamagana timu ya soka ya Nyamwaga fc imeishapa bila huruma timu ya
Eleven hunter kwa uma ya bao 4-3 katika mchezo mkai uiopigwa Uwanjani hapo.
Katika
mchezo huo uliokuwa mkani na wa piga ni kupige ulishuhudia timu zote zikicheza
kwa ushindani mkubwa huku timu hizo zikipokezana kufungana mabao ambapo
Nyamwaga fc ndio walitangulia kufunga mabao mawili lakini yakachomolewa na
kufunga mabao mengine jambo ambalo liliwafanya eleven hunter kushindwa
kurudisha mabao hayo na ujiuta wakipokea kichapo cha bao 4-3 katika mchezo huo.
Akizungumza
na mtandao huu Kocha mkuu wa Nyamwaga fc Kessy Mziray amesema kuwa licha ya
kupata ushindi katika mchezo huo , mchezo ulikuwa mgumu kwa upande wa timu yake
" mchezo wa leo kiukweli ulikuwa mgumu kutokana na aina ya timu
tuliyocheza nayo kwani walijaribu kutuiga mfumo wetu na wakafanikiwa lakini kwakua
sisi ni wazoefu tuliwafunga tena hivyo nawapongeza vijana wangu" alisema
kwa upande
wake Kocha mkuu wa Eleven Hunter ambaye alishindwa kutaja jina lake kutokana na
kipigo hicho alisema kuwa walitarajia kuifunga Nyamwaga lakini ndio mchezo
" tulikuwa tunacheza na timu ngumu ambayo haijawahi kupoteza mchezo wowote
katika mashindano haya hivyo tumekubali matokeo na tunakwenda kujipanga
kuelekea mchezo ujao" alisisitiza.