Timu ya soka ya Pamba Sports Club ya jijini hapa imeendelea kufanya maandalizi ya ushiriki wa ligi daraja la kwanza baada ya kuichapa timu ya Iseni fc kwa bao 5-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijin hapa.
Kocha mkuu wa Pamba SC Mathias Wandiba Master amesema kuwa lengo la kucheza michezo mingi ni kuhakikisha kuwa timu inapata maandalizi ya kutisha kabla ya ligi kuanza " sisi Pamba tumeamua kucheza michezo mingi ya kirafiki ili wachezaji waelewane kabla ya ligi kuanza hivyo mipango yetu ni kupanda daraja kucheza ligi kuu.