TOTO AFRICAN KUMENYANA NA ELEVEN STARS KOMBE LA FA

Desemba 19, 2017
Timu ya soka ya Toto african ya jijini Mwanza inayoshiriki ligi daraja la kwanza kundi C kesho desemba 20 mwaka huu inatarajia kucheza mchezo wake wa kombe la shirikisho maarufu kama kombe la FA dhidi ya Eleven stars ya mkoani  Kagera  ambapo mchezo huo utapigwa Uwanja wa Nyamagana kuanzia majira ya saa 10 za jioni.

mwenyekiti wa timu hiyo Godwin Aiko amewaomba wapenzi na wadau wa timu hiyo kuhakikisha kuwa wanaokeza kuipa sapoti katika mchezo huo " timu yetu kesho itacheza na Eleven stars kutoka Kagera katika kombe la FA hivyo wadau wajitokeze kuisapoti timu yao kwani tumejipanga kushinda" alisema

POGBA ARUDI KIVINGINE AIWEZESHA MAN U KUICHAPA NEWCASTLE

Novemba 18, 2017
Timu ya Manchester United imeichapa timu ya Newcastle jumla ya bao 4-1 katika mchezo wa ligi kuu nchini England mchezo uliopigwa Uwanja wa Old traford jijini Manchester, Mabao ya washindi katika mchezo huo yalitiwa kimiani na Antony Martial dakika ya 37,Chris Smalling dakika ya 45, Paul Pogba dakika ya 54 huku Romelu Lukaku akihitimisha kalamu ya mabao dakika ya 71 ya mchezo huo huku bao la kufutia machozi kwa newcastle likifungwa na D.Gayle dakika ya 14 ya mchezo huo.
Matokeo mengine katika ligi kuu nchini England
Arsenal 2-0 Totenham
Leicester city 0-2 Manchester City
West browhich 0-4 Chelsea
Crystal Palace 2-2 Everton
Liverpool 3-0 Southampton
Burnley 2-0 Swansea city
AFC Bournemo 4-0 Huddersfield town

SIMBA YAVUNJA MWIKO MBEYA, YAITANDIKA PROSON

Novemba 18, 2017
Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam imevunja mwiko baada ya kuitandika timu ya wajelajela wa Mbeya Tanzania prison kwa jumla ya bao 1-0 bao lililofungwa dakika ya 88 na mshamuliaji wa timu hiyo John Bocco baada ya mchezo huo Simba imefikisha jumla ya pointi 22 baada ya michezo 10 hata hivyo wachambuzi wa maswala ya kisoka hapa nchini wanasema kuwa Klabu ya Simba ikipata ushindi katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huwa inatwaa Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, hata hivyo ikumbukwe kuwa msimu uliopita Simba walifungwa bao 2-0 na Prison

Matokeo mengine katika ligi kuu leo 
Majimaji 2-1 Mbao Fc 
Tanzânia prisons 0-1 Simba Sports Club 
Ruvu shooting 1-0 Ndanda Fc 
Stand United 0-0 Mwadui Fc

HABARI FC YAICHINJA OPEN UNIVERSITY

Novemba 10, 2017
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo Jijini Mwanza maarufu kama Habari fc jana ilifanikiwa kuibugiza timu ya Chuo kikuu huria cha jijini Mwanza kwa jumla ya bao 5-3 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali ulishuhudia Mabao ya Habari fc yakifungwa na Juma Ayo aliyefunga mabao mawili katika mchezo huo huku mabao mengine yakifungwa na Ramadhan. Mara baada ya mchezo huo timu ya Habari fc inaendelea na maandalizi yake katika kuelekea michezo mingine ya kirafiki.

MWANZA STARS VETERAN YAICHAPA TIMU YA WAANDISHI WA HABARI KWA TAABU SANA

Oktoba 22, 2017
Timu ya soka ya Mwanza starS Veteran imefanikiwa kuichapa timu ya wanahabari za Michezo mkoani Mwanza kwa jumla ya bao 7-6 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza , katika mchezo huo ulioshuhudia wachezaji wa timu ya Mwanza Stars veteran wakitumia muda mwingi kupoteza muda lakini walifungwa mabao yote kabla ya kusawazisha na kufunga bao la ushindi, mara baada ya mchezo huo Kocha mkuu wa Mwanza stars Veteran Ibrahim Murumba amesema kuwa lengo kuu la mchezo huo ni kuongeza mahusiano baina ya waandishi wa habari na wachezaji hao wa zamani " sisi kama wachezaji wa zamani tumeamua kucheza mchezo huu na watoto wetu waandishi wa habari mchezo ulikuwa mzuri na tumejivunia sana kucheza mchezo huu" alisema

Kwa upande wake nahodha wa timu ya wandishi wa habari za michezo mkoa wa Mwanza Moses William amesema kuwa timu ya Mwanza stars veteran wameshinda kwa mbinde " kimsingi hawa wachezaji wa zmani tuliocheza nao leo wametufunga kwa mbinde lakini kazi yetu wameiona hivyo sisi tutaendelea na maandalizi yetu kuhakikisha kuwa tunacheza nao tela ili na sisi tulipe kisasi
Mara baada ya mchezo huo Uongozi wa timu ya wanahabari fc unajiandaa kucheza mchezo na timu ya Bunge mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma bada ya mazungumzo kukamilika.

PAMBA SC YALAANI KITENDO CHA WATU KUUKATA UWANJA WA NAMAGANA

Oktoba 16, 2017
Octoba 14 mwaka huu  Klabu ya Soka ya Pamba sc ilicheza na Toto African mchezo wa Ligi daraja la kwanza kundi C  na mchezo huo kumalizika Kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Kabla ya mchezo huo kulikua na taarifa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watu wasiojulikana wameingia katika Uwanja wa nyasi bandia wa Nyamagana uliopo katikati ya Jiji la Mwanza  na kukata sehemu ya uwanja huo hali iliyopelekea uwanja huo kuwa na sehemu yenye tundu katika uwanja huo ambapo badae Ofisa michezo wa Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko ambaye pia ni  Msimamizi wa Uwanja huo  alithibitisha kutokea Kwa tukio  hilo na kusema kuwa hatua Kali zitachukuliwa Kwa watakaobainika kuhusika na kitendo hicho cha kuukata uwanja wa Nyasi bandia wa Nyamagana.
Sisi kama klabu ya Soka ya Pamba SC tunalaani vikali tukio hilo kwakua siyo tukio la kiungwana Kwa Soka letu kwani Uwanja wa Nyasi bandia wa Nyamagana  umetumia muda zaidi ya miaka 2 kukamilika na uwekezaji wa fedha nyingi umetumika hivyo tunalaani tukio hilo la kukatwa Kwa sehemu ya Uwanja wa Nyamagana na tunaomba watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho Kwa wengine hivyo Pamba SC inalaani vikali kitendo hicho ambacho kimelidhalilisha Soka letu Kwa kuamini imani za kishirikina kuliko maandalizi ya timu.
Lakini pia Klabu ya Pamba inakanusha vikali kuhusika na tukio hilo ambalo sio la kiuana michezo katika nchi yetu.
Picha chini inaonyesha sehemu ya Uwanja wa Nyamagana  iliyokatwa

TOTO AFRICAN YALAZIMISHA SARE NA PAMBA SC

Oktoba 14, 2017
Wakati ligi daraja la kwanza ikiendelea kutimua vumbi timu ya soka ya Toto african imelazimisha kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Pamba sc zote kutoka jijini Mwanza, mchezo huo umeshuhudia wakazi wa Mwanza wakishuhudia burudani ya aina yake huku Pamba sc wakionyesha mchezo mzuri katika ligi hiyo iliyoendelea leo Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza licha ya kushindwa kuibuka na ushindi wa pointi 3 muhimu  baada ya mchezo wa hii leo Pamba imefikisha jumla ya pointi 3 baada ya michezo 5 hivyo bado iko nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi daraja la kwanza kundi C huku Timu ya Alliance schools ambayo itashuka dimbani kesho kumenyana na Transit Camp ikiwa na Pointi 10 kileleni. hata hivyo rekodi tangu timu hizi zikutane mchezo wa september 14 2013 Toto iliifunga Pamba bao 1-0 na marudio february 22 2014 Pamba nao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano  wa ligi daraja la kwanza. lakini mwaka 2016 Pamba ilifungwa na Toto bao 4-1 katika michuano ya kombe la FA na leo october 14 2017 timu hizi zimetoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Nyamagana.

YANGA WALIVYOTUA BUKOBA KUWAVAA KAGERA SUGAR

Oktoba 13, 2017

Klabu ya soka ya Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu bara, tayari mewatua mkoani Kagera kwa maandalizi ya mchezo wao na Kagera Sugar utakaopigwa kesho Jumamosi Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana kwenye uwanja huo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao  6-2 katika msimu wa mwaka jana

Credit Picha na Faustine Ruta.

TOTO AFRICAN VS PAMBA SC DERBY YA KIBABE JIJINI MWANZA

Oktoba 13, 2017



Octoba 14 mwaka huu Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza zitamenyana timu za Toto Africa pamoja na timu ya Pamba sc zote za jijini Mwanza, timu hizo kwa sasa ziko ligi daraja la kwanza kundi C ambapo mpaka sasa kila timu imecheza jumla ya michezo 4 ambapo Toto African wao wanajumla ya pointi 4 huku Pamba sports Club wao wakiwa na jumla ya pointi 2 na kushika mkia katika kundi C. Kuelekea mchezo huo championi limekuletea baadhi ya mambyoa mabyo huenda yatatokea katika mchezo huo.

PAMBA KUTUMIA UKONGWE.
Mara zote kuelekea katika mchezo unazokutanisha timu ya Toro African na Pamba sc mchezo huu huwa mgumu kutokana na historia ya timu hizi mbili, kwanza Klabu ya soka ya Pamba ndiyo klabu kongwe kuliko timu ya Toto African ambapo Pamba imeanzishwa mwaka 1968 mbele ya Uwanja wa CCM Kirumba huku Toto African yenyewe ikianzishwa mwaka 1972 hivyo kutokana na Ukongwe huo Pamba sc inapewa nafasi ya kuweza kuushinda mchezo huo lakini wachambuzi wa maswala ya soka wanasisitiza kusubiri dakika 90 ziweze kuamua.

Rekodi zinambeba Pamba SC
Klabu ya soka ya Pamba sc ambayo ilianzishwa mwaka 1968 imewahi kutwaa Ubingwa wa ligi kuu bara mwaka 1990 enzi hizo ligi daraja la kwanza  lakini pia mwaka 1989 na mwaka 1992 timu hiyo pia ilitwaa Ubingwa wa michuano ya Nyerere Cup ambapo Pamba fc ilipata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa kabla ya kushuka daraja rasmi mwaka 2000 ambapo haijapanda daraja mpaka leo hivyo Pamba kama ikitumia uzoefu wake katika mashindano huenda ikapata pointi katika mchezo huo ambao utakuwa mkali na wa aina yake kwa timu zote mbili kutokana na historia iliyopo.

Toto African Panda shuka
Klabu ya Toto African ni miongoni mwa timu zeye bahati na ligi kuu bara lakini baadhi ya wadau wake wasioitakia mema wamekuwa wakiishusha daraja lakini pia kitendo cha timu hiyo  kuwa katika ligi kuu bara na kupania mchezo wake na Simba huwa kinawakera wadau wengi wa soka jambo linaloifanya timu hiyo ishindwe kujitengenezea mazingira ya kusalia kwenye ligi na tangu timu ya Pamba sports Club ishuke daraja Toto African imecheza ligi kuu bara ikipanda daraja na kushuka kwa zaidi ya misimu mitatu hivyo kutokana na Toto African kuwa na uzoefu mkubwa katika ligi hiyo  inaweza kupata matokeo katika mchezo huo japokuwa soka la timu hizi mbili huwa halitabiriki.

Rekodi ya timu hizo zilipokutana.
Kwa mujibu wa aliyekuwa Kocha mkuu wa timu ya Pamba Venance Kazungu ambaye amehudumu katika timu hiyo kwa muda mrefu ameliambia gazeti hili kwamba katika michezo mingi ambayo timu za Toto African na Pamba , Klabu ya Pamba imekuwa ikipata matokeo mara nyingi zaidi kuliko pamba ambapo katika msimu wa mwaka 2013/14 timu hizo zilipokuwa ligi daraja la kwanza kundi C  timu hizo zilikunata septemba 14 ,2013 timu ya Toto African ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lakini pia timu hizo ziliporudiana sebruari 22 mwaka 2014 timu ya Pamba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na msimu wa mwaka 2016/17 timu hizo zilikutana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo wa kombe la FA na Toto iliifunga Pamba bao 4-1 hivyo mchezo wa timu hizo utakuwa mkali na wakusisimua.

Toto African vs Pamba derby ya tatu Tanzania
Ukiachana na Derby ya Simba na Yanga ambayo ndiyo derby ya tatu barani Africa  baada ya ile ya nchini Misri ya Al ahly vs zamaleck na Orlando Pirates vs KaizerChiefs ya Afrika kusini  , katika nchi yetu Derby ya pili ni ile ya African Sports dhidi ya Coastal Unioni na derby ya tatu ni Pamba dhidi ya Toto African hivyo kutokana na ukumbwa huo mchezo wa timu hizo utakaopigwa Otoba 14 mwaka huu Uwanja wa Nyamagana jijini hapa utakuwa na ushindani wa aina yake.

Vikosi vya timu zote mbili.
Kuelekea mchezo wa timu za Pamba dhidi ya Toto African vikosi vyote viko katika hali nzuri kwani timu hizi zinaelekea katika mchezo huo huku Toto African wakiwa na jumla ya pointi 4 huku Pamba sc wao wakiw ana pointi 2 pekee baada ya michezo 4 hivyo kikosi kitakachojiandaa vizuri ndicho kitakachopata matokeo kwani timu hizi huwa hazikutani mara kwa mara na badala yake kukutana kwake mpaka matukio maalumu kama hivi ligi daraja la kwanza.

Mashabiki wa timu zote mbili.
Mpaka sasa timu ya soka ya Pamba ambayo iliwahi kutamba hapo nyuma katika soka la nchi hii imewapoteza mashabiki wake baada ya kuanza vibaya michuano hii ya ligi daraja la kwanza hivyo endapo itafanya vizuri katika mchezo wake a Toto, itaendelea kukuza mtaji wake wa mashabiki lakini pia Toto African nao wakipata ushindi wataendelea kuw ana mtaji wa mashabiki waliokuwa nao kwani timu hiyo imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja huku ikipoteza michezo 2 hivyo timu yoyote itakayofungwa katika mchezo huo itakuwa imepoteza ramani ya kufanya vema katika ligi daraja la kwanza ikiwa ni pamoja na kupanda daraja kuelekea ligi kuu.

ALLIANCE WALIMWA FAINI LICHA YA KUFANYIWA FUJO TABORA

Septemba 28, 2017
Mechi namba 2 Kundi C (Rhino Rangers v Alliance).
Timu ya Alliance imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kutoingia vyumbani wakati wa ukaguzi na wakati wa mapumziko, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Daraja la Kwanza, na adhabu imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Pia viongozi wa benchi la ufundi la Alliance, Kocha Msaidizi Kessy Mziray, Kocha wa makipa Tade Hussein, Mtunza vifaa Josephat Munge na Meneja wa timu James Bwire wamepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kila mmoja kwa kosa la kumbughudhi mwamuzi wakimtaka kumaliza mpira kabla ya muda wakidai muda umekwisha wakati kazi ya kutunza muda si yao. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Rhino Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) na barua ya Onyo kutokana na mashabiki wa timu hiyo kufanya fujo baada ya mechi kumalizika. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza.

MENEJA PAMBA SC AFUNGIWA MWEZI KUKAA KWENYE BENCHI

Septemba 28, 2017
Mechi namba 4 Kundi C (Dodoma FC v Pamba). Meneja wa timu ya Pamba FC, Salmin Kamau amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mwezi mmoja kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa mwamuzi. Adhabu dhidi yake imezingatia Kanuni ya 41(2) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Viongozi.
 
Lakini pia Klabu ya Pamba imekuwaje  Meneja wake Salmini Kamau afungiwe wakati waamuzi waliochezesha hovyo katika mchezo huo hawajachukuliwa hatua "haiwezekani Meneja wetu afungiwe wakati mwamuzi aliyecheza mchezo wa Dodoma fc na Pamba sc Clement Ntambi ambaye kimsingi alichezesha kwa viashiria vya maelekezo asichukuliwe hatua hivyo klabu ya Pamba itajua nini cha kufana kuhusu hilo" alisema kiongozi wa Pamba baada ya kupata taariffa kutoka TFF.

KOCHA MKUU TOTO AFRICAN ABWAGA MANYANGA

Septemba 27, 2017



Siku moja baada ya timu ya Toto African kutoka sare ya kutofungana na timu ya Alliance sports academy katika mchezo wa nligi daraja la kwanza mchezo uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini hapa aliyekuwa Kocha mkuu wa Toto African Almas Mosh ametangaza kujiuzulu wadhifa wake katika timu hiyo.

Mosh ameliambia championi kuwa sababu kubwa iliyopelekeaq yeye kubwaga manyanga katika tiomu hiyo ni kutokana na timu yake aliyokuwa akiitumikia kushindwa kumlipa nstahikizake “ Mim I nimeam,ua kujuzulku nafasi yangu ndani ya Toto African kutokana na waajiuri wangu kusdhindwa kunilipa stahiki zangu  jambo ambalo limenivunja moyo na kushindwa kuendelea kuifundisha timu hiyo” alisema

Aidha Mosh amesema kuwa tangu akabidhiwe mikoba ya kuifundisha timu hiyo tangu ishuke daraja hajawahi kupewa maslahi yake hali iliyopelekea ajiuzulu kuifundisha timu hiyo “ Mimi nimekabidhiwa mikoba ya kuiufundisha Toto African na usajili nimefanya mwenyewe lakini mwisho wameshindwa kunilipa hata mshahara wangu hivyo kuanzia leo mimi sio kocha wa Toto African “ alisema

Alipotafutwa  mwenyekiti wa timu ya Toto African Godwin Aiko ili kujibu taarifa hizo siku yake ya mkononi iliita bila kupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya sms hakuweza kujibu ikumbukwe kuwa Kocha Almas Mosh ameiongoza Toto African katika michezo miwili ambapo mchezo wa kwanza timu hiyo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Biashara fc ya mkoani Mara na mchezo wa pili timu hiyo ikatoka sare ya kutofungana na Alliance sports academy hivyo mpaka sasa timu hiyo ina jumla ya pointi 1 katika  michezo 2 iliyocheza.

Credit: Championi.

PAMBA ILIVYOTOKA SARE NA JKT OLJORO

Septemba 24, 2017

Klabu ya soka ya Pamba sc jana ilifanikiwa kutoka sare ya kutofungana na timu ya JKT Oljoro katika mchezo wa ligi daraja la kwanza mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro, katika mchezo huo Pamba wanapaswa kujilaumu wenyewe kwani wachezaji wake walikosa nafasi nyingi za wazi ambazo kama wangefunga wangeibuka na ushindi wa pointi tatu, Mpaka sasa Pamba SC imecheza jumla ya michezo 2 imefungwa mmoja na kutoka sare mchezo mmoja lakini pia JKT Oljoro wao wamecheza michezo miwili pia na wametoka sare michezo yote , Pamba itacheza tena octoba 2 kwenye Uwanja wa Nyamagana ambapo itamenyana na timu ya Biashara fc kutoka mkoani Mara.

Aidha katika mchezo wa Pamba dhidi ya Jkt Oljoro ulishuhudia timu ya JKT oljoro wakichelewa kufika Uwanjani ambapo hapo awali mchezo huo uliokuwa uanze saa 10: 00 jioni ulichelewa kuanza kutokana na timu wenyeji kuchelewa kuingia Uwanjani ambapo waliingia Uwanjani saa 10: 15 hali iliyosababisha mchezo huo kuanza kutimua vumbi saa 10:25 jioni.
Lakini pia mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mwanza Vedastus Lufano alifika Uwanjani hapo kuishuhudia Pamba ikicheza na JKT Oljoro.

NYEGEZI TERMINAL WANZA VYEMA NDONDO CUP WAICHAPA BUZURUGA TERMINAL

Septemba 20, 2017
Yale mashindano ya Ndondo Cup katika mkoa wa Mwanza yameanza kutimua vumbi leo septemba 20 kwenye Uwanja wa Nyamagana ambapo katika mchezo wa Ufunguzi uliozikutanisha Nyegezi Terminal na Buzuruga Terminal umemalizika kwa Nyegezi Teriminal kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo ulioshuhuiwa na mamia ya mashabiki, Buzuuruga Terminal walikuwa na jezi ya Rangi nyekundu huku Nyegezi terminal wakiwa na jezi ya Blue katika mchezo huo, mgeni rasm katika ufunguzi wa mashindano hayo alikuwa ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.