SIMBA ,YANGA KUSHIRIKI SPOTPESA CUP KENYA

Mei 17, 2018

Timu za Simba, Yanga , Singida United na JKU inayoshiriki ligi kuu nchini Zanzibar zinatarajia kushiriki michuano ya Sportpesa ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hizi katika michuano itakayofanyika Nairobi nchini Kenya,

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Spotpesa hapa nchini Abas Tarimba amesema kuwa michuano hiyo juni 3 mwaka huu nchini Kenya ambapo bingwa wa kombe hilo atasafiri kwenda nchini Uingereza kucheza na timu ya Everton na safari hiyo itaghalamikiwa kila kitu.

na bingwa wa Sporpesa kwa mwaka huu atajipatia zawadi ya fedha taslimu dola elfu thelathini

Ikumbukwe kuwa mwaka jana michuano ya Spotpesa ilifanyika hapa nchini na bingwa akawa Gormahia ya nchini Kenya ambapo walipata nafasi ya kucheza na Evertone inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

PICHA JINSI ATLETICO MADRID ILIVYOTWAA UBINGWA WA UROPA

Mei 17, 2018

Timu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Uefa Uropa League baada ya kuitandika timu ya Olympic Masseile kwa jumla ya bao 3-0 huku mshambuliaji hatari wa Ufaransa Antoine Greizman akifunga mabao mawili katika fainali hiyo huku bao la tatu likifungwa na nahodha wa timu hiyo Gabi dakika ya 90 ya mchezo huo, Olympic Maseile ilitinga katika fainali ya michuano hiyo baada ya kutinga katika fainali kama hiyo mwaka 2004.

zifuatazo ni picha zinavyoonyesha hali ilivyokuwa katika Fainali hiyo.




















 Nahodha wa kikosi cha Olympic Masseile Demitty Payet akitoka nje ya Uwanja  baada ya kuumia katika fainali hiyo

 Antonio Greizman akifunga bao

 Mshambuliaji wa Atletoco Madrid Antoine Grezman akishangilia moja ya bao alilofunga.

KIKOSI CHA YANGA KUELEKEA MECHI NA RAYON SPORTS

Mei 16, 2018

NIGERIA YATANGAZA KIKOSI CHAO KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

Mei 16, 2018

Shirikisho la soka nchini Nigeria limetangaza majina 30 ya wachezaji watakaoiwakilisha nchi yao katika mashindano ya kombe la dunia linalotarajia kuanza kutimua vumbi juni 14 Moscow nchini Urusi na katika kikosi hicho cha wachezaji 30 kinatarajia kuchezwa na kubaki wachezaji 23 ambao majina yao yanatakiwa kuwasilishwa kwenye shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA kabla ya tarehe 4 mwezi juni mwaka huu.

kikosi kamili kilichotajwa hiki hapa

Goalkeepers: Ikechukwu Ezenwa (Enyimba FC), Francis Uzoho (Deportivo La Coruna, Spain), Daniel Akpeyi (Chippa United, South Africa), Dele Ajiboye (Plateau United).
Defenders: Abdullahi Shehu (Bursaspor FC, Turkey), Tyronne Ebuehi (Ado Den Haag, The Netherlands), Olaoluwa Aina (Hull City, England), Elderson Echiejile (Cercle Brugge KSV, Belgium), Brian Idowu (Amkar Perm, Russia), Chidozie Awaziem (Nantes FC, France), William Ekong (Bursaspor FC, Turkey), Leon Balogun (FSV Mainz 05, Germany), Kenneth Omeruo (Kasimpasa FC, Turkey), Stephen Eze (Lokomotiv Plovdiv, Bulgaria).
Midfielders: John Obi Mikel (Tianjin Teda, China), Ogenyi Onazi (Trabzonspor FC, Turkey), Wilfred Ndidi (Leicester City, England), Oghenekaro Etebo (UD Las Palmas, Spain), John Ogu (Hapoel Be’er Sheva, Israel), Uche Agbo (Standard Liege, Belgium), Joel Obi (Torino FC, Italy), Mikel Agu (Bursaspor FC, Turkey).
Forwards: Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia), Kelechi Iheanacho (Leicester City, England), Moses Simon (KAA Gent, Belgium), Victor Moses (Chelsea FC, England), Odion Ighalo (Changchun Yatai, China), Alex Iwobi (Arsenal FC, England), Nwankwo Simeon (Crotone FC, Italy), Junior Lokosa (Kano Pillars). 

BARCELONA WATUA AFRIKA KUSINI KUMUENZI MANDELA

Mei 16, 2018

Klabu ya soka ya Barcelona ya nchini Hispania mapema leo imewasili nchini Afrika kusini ambako inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mamelod Sundown mchezo ambao utakuwa maalumu kwaajili ya kumuenzi aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nelson Mandela ambapo mchezo huo unatarajia kuchezwa leo jioni majira ya saa 1 usiku katika Uwanja wa FNB uliopo nchini Afrika kusini.

hata hivyo kama ambavyo haikutarajiwa timu ya Barcelona imeingia nchini Afrika kusini huku ikiwa na nyota wake wote akiwemo Lionel Messi, Luis Suarez pamoja na Andres Iniesta anayepanga kustaafu kuichezea timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.





Pep Guardiola says Man City will sign 'one or two' players as club must curb high spending

Mei 16, 2018


Fresh from breaking the all-time points tally for a Premier League season, Guardiola said City will aim to bring in "one or two" new additions during the summer.
They spent £278m on nine players during 2017/18, including Kyle Walker, Bernardo Silva and Ederson, and there had been questions whether the likes of Manchester United, Spurs and Chelsea could match such significant amounts.
But Guardiola told Monday Night Football City themselves will avoid spending similar figures in future - because they can't afford it.
"[We will sign] one or two more, no more," he said. "We cannot invest…maybe people don't believe me but we don't have the money to invest £300m every season.
We invested a lot of money and will invest less in the future, because instead of doing it in two or three transfer windows, we did it in one. We needed it for the age [of the squad].
"The fundamental success of this season is the quality of the players. People say you won because you invest a lot, they are right.

Yaya Toure will leave the club in the summer following the expiration of his contract at the Etihad, and central midfield is one of the positions Guardiola is targeting to recruit before the start of next season on August 11.
In addition to Toure's replacement, the Spaniard was coy on where else City would look to strengthen.
He said: "Maybe in front, but I don't know. We have to think and talk more with Txiki and the staff. It's four competitions, we need new faces to compete with the guys from this season."

Credits: Kysports

BRAVOO YANGA, KILA LA KHERI DHIDI YA RAYON SPORTS

Mei 16, 2018

Kuna habari nyingi sana huwa zinanichanganya kichwa, habari ambazo huwa zinanifanya niwaze.
Tafakuri yangu huchukua muda mrefu sana lakini majibu yake huwa tofauti na mitazamo ya walio wengi.
Ndimi za watu wengi zinakiri kuwa ligi yetu ni ngumu, ndimi hizi huwa zinanichosha pale zinapohubiri ugumu wa ligi yetu kutokana na ushindani unaoonekana kwenye ligi yetu.
Ligi ambayo haina wadhamini wengi wa kutosha, ligi ambayo vilabu vyake vinalia njaa kwa sababu ya kushindwa kujiendesha kibiashara.
Ligi ambayo haina makocha ambao wana elimu kubwa ya kufundisha mpira na makocha wasiopenda kujifunza mabadiliko ya mpira wa kisasa.
Ligi ambayo ina viongozi wanaoongoza vilabu vyao katika misingi ya kijamaa, bakuri ndiyo huwa msaada tosha katika kuendesha timu zao, bakuri ambalo halina ujazo wa motisha kwa wachezaji.
Nguvu za kupigana huishia nje ya uwanja kwa sababu hakuna kinachowafanya wapigane kwa nguvu.
Ndipo hapo vilabu vya Simba na Yanga vinapochukua upenyo wa kubadilishana makombe.
Ni vilabu vikongwe, haviendeshwi katika misingi ya kisasa lakini vina watu ambao huvipenda kwa dhati mpaka kufikia hatua ya kujitolea pesa zao ili kuiimarisha timu yao kwa msimu husika.
Usajili unaofanyika huwa unafanyika katika viwango vya kawaida, wachezaji wanaoletwa Simba na Yanga huwa hawapishani kwa kiasi kikubwa na wachezaji wa timu zingine, kinachowatofautisha ni huduma tu.
Huduma ndiyo huamua nani ni bingwa wa ligi yetu na ninani anastahili kushuka daraja.
Mwenye huduma  nzuri katika msimu husika ndiye ambaye huwa na uwezo mkubwa wa kuchukua kombe la ligi kuu ya Tanzania.
Hatua inayofuata ndiyo huwa inakuwa kichekesho kwa mwakilishi wetu wa mechi za vilabu vya kimataifa.
Hutia aibu, hutia simanzi na hutia huruma ambayo hugeuka kuwa mshangao, na nirahisi sana kujiuliza maswali yenye mshangao mkubwa ndani yako unapomuona bingwa wa nchi yako anaposhindwa kupambana na bingwa wa nchi nyingine tena kwa kupokea kipigo cha fedhea!.
Ndipo hapo akili yangu inapokuja kujihoji swali moja, iko wapi ligi ya ushindani tunayoihubiri?, uko wapi ubora wa ligi yetu kama timu zetu haziwezi kushindana na timu zenye nguvu katika michuano ya CAF?
Jibu ni jepesi tu, ligi yetu inampata bingwa kutokana na utofauti wa huduma iliyopo ndani ya Simba, Yanga na vilabu vingine.
Hakuna ubora uliopo kwenye ligi yetu, hata hizi timu ambazo tunazihubiri ni kubwa na ni bora hazina vikosi imara vya kushindana katika mashindano ya kimataifa.
Vikosi vyao vina wachezaji ambao wana uwezo wa kushindana katika michuano yetu ya ndani tu, michuano ambayo hupeleka mwakilishi kwenye michuano ya kimataifa, mwakilishi ambaye hana kikosi imara cha kushindana kwenye michuano hiyo ya kimataifa.
Hapo ndipo mwanzo wa kutengeneza uongo wa kutufurahisha unapoanza. Uongo huu huanza kutufurahisha kumuona Emmanuel Okwi anapoifunga Azam Fc timu ambayo haina kikosi imara kama timu tunazokutana nazo katika mechi za kimataifa.
Uongo huu hutufurahisha kweli na cha ajabu hututia upofu na kushindwa kuona wenzetu wanavyofanya usajili imara kwa ajili ya michuano hii ya kimataifa.
Tabia yetu ya kusajili kwa mazoea huendelea, tunasajili mchezaji kutokana na matakwa ya mtu na siyo kulingana na matakwa ya benchi la ufundi, ndipo hapo tunapojaza wachezaji wa kawaida katika vilabu visivyo vya kawaida.
Yanga ya jana ilikuwa Yanga iliyojaza wachezaji wa kawaida katika klabu isiyo ya kawaida.
Wachezaji ambao hawana ushindani, hapana shaka walienda Algeria kwa ajili ya kupunguza idadi ya magoli ya kufungwa.
Hawakuwa na wachezaji wa kushindana kwa nguvu ili kupata alama katika uwanja wa nyumbani.
Wote walikuwa wakiwa kama makinda ya ndege yaliyoachwa na mama yao bila msaada wowote.
Hakukuwepo na kiongozi kuanzia katika benchi la ufundi mpaka ndani ya uwanja. Idara zote tatu (ulinzi, kiungo na ushambuliaji) zilikosa mtu wa kuongoza.
Safu ya ulinzi ilikuwa inashindwa jinsi ya kukaa na kujilinda nyuma ndiyo maana magoli yao waliyofungwa yalikuwa ni kwa sababu ya ‘marking’ mbovu.
Hata kuanzisha mashambulizi walinzi walishindwa, viungo wakakosa cha kufanya hali iliyowafanya washambuliaji wakose cha kutenda.
Hakukuwepo na kiongozi yoyote wa kuwaongoza ili wafanye maamuzi yaliyokomaa uwanjani, hakukuwepo na mchezaji wa kuibeba timu kuanzia golini mpaka kwa mshambuliaji.
Na kibaya zaidi hata benchi la ufundi walishindwa kipi wanatakiwa kufanya kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho wa mchezo, timu ilikuwepo pale kukamilisha dakika 90 tu bila mpango wowote wa kutoka na alama yoyote.
Credits: Tanzania sports

PAMBA SC KUKUTANA MEI 20

Mei 16, 2018

Klabu ya soka ya Pamba Sc inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara inatarajia kuwa na Mkutano wake utakaofanyika Mei 20 mwaka huu kuanzia majira ya saa 9:00 Alasiri ambapo utafanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Aden Palace iliyoko wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Lengo kuu la Mkutano huo ni kujadili mwenendo na Maandalizi kuelekea ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao ambapo wahusika katika mkutano huo ni pamoja na Wachezaji wa Zamani wa Pamba Sc, Wadau, wapenzi na mashabiki wa timu ya Pamba ambayo imekuwa na historia kubwa katika soka la Nchi yetu.

Mnaombwa kufika bila kukosa katika mkutano huo ambao ndio utakaotoa Mustakabali wa timu yetu kushiriki ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao na hatimaye kupanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara.

LICHA YA UKATA , FANTOM YAENDELEA KUWA MWIBA LIGI YA MABINGWA

Mei 11, 2018
Timu ya soka ya Fantom fc ya jijini Mwanza ambao ndio mabingwa wa soka katika mkoa huu wamefanikiwa kupata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Nyamongo fc ya mkoani Mara katika mchezo wa ligi ya mabingwa kituo cha Geita katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Shule ya sekondari waja iliyopo mkoani Geita

mara baada ya mchezo huo Mtandao huu umezungumza na kocha mkuu wa Fantom Mathias Wandiba ambapo amesema kuwa malengo yake ni kuhakikisha kuwa anapata pointi katika kila mchezo " tunamshukuru Mungu kwa matokeo tuliyopata tutaendelea na maandalizi yetu ili tuweze kuendelea kufanya vyema zaidi" alisema

ikumbukwe kuwa jana kulikuwa na taarifa kuwa timu hiyo ya Fantom imefukuzwa katika hoteli waliyokuwa wakiishi kutokana na ukata unaoikabili timu hiyo na hii leo timu hiyo imepata msaada wa fedha taslimu shilingi 240000 kutoka kwa chama cha soka mkoa wa Mwanza kwaajili ya malipo ya marazi kwa wachezaji.

COPCO VETERAN NI GARI LIMEKOLEA YAPIGA MTU BAO 12-0

Machi 24, 2018
Ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Mwanza kwa sasa mambo ni moto baada ya timu ya Copco Veteran kuishushia kichapo kikali cha bao 12-0 timu ya Vijana fc ya Misungwi  katika mchezo wa ligi uliofanyika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa, kwa sasa Copco wameongeza Presha kwa timu ya Phantom ambayo inapointi 15 katika ligi hiyo huku Copco wao wakishika nafasi ya pili baada ya kuwa na pointi 11  hivyo kwa sasa ligi hiyo inachezwa saa nane mchana pamoja na saa 10 jioni ili kuwahi karenda ya Shirikisho la soka hapa nchini TFF ambayo inaitaka mikoa yote hapa nchini kuwakilisha jina la bingwa kwenye shirikisho hilo ili kuanza maandalizi ya ligi ya mabiingwa mikoa.

MBAO FC YATESTI MITAMBO YAKE YAMPIGA MTU 7-2 CCM KIRUMBA

Machi 23, 2018
Timu ya Mbao fc ya jijini Mwanza inayoshiriki ligi kuu Tanzania bada imeichapa bila huruma timu ya Marsh fc kwa jumla ya bao 7-2 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jioni ya leo, mchezo huo ulikuwa maalum kwa Mbao fc kujipima nguvu baada ya timu hiyo kuonekana ikisuasua katika ligi.

Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Mbao fc Ettiene Ndayiragije amesema kuwa aanaendelea kukisuka upya kikosi chake ili aweze kufanya vyema katika michezo nane iliyosalia " tumeshinda mchezo huu wa kirafiki na nitaendelea kuwanoa vijana wangu ili waweze kuiongoza timu yao kufanya vyema katika ligi na tunaamini tutafanya maajabu katika michezo ya ligi iliyobaki" alisema

Kwa sasa Mbao iko katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu bara baada ya kuwa na pointi 19 baada ya kucheza michezo 22.

PHANTOM HAISHIKIKI LIGI DARAJA LA TATU MWANZA

Machi 23, 2018
Timu ya Phantom fc ya wilayani Nyamagana jijini hapa imekuwa mwiba mkali katika ligi daraja la tatu mkoa wa Mwanza baada ya kuichapa timu ya Ndovu fc kutoka wilayani Ilemela kwa bao 5-1 katika mchezo uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa, katika mchezo wa awali timu ya Copco veteran imeichapa Singa fc ya Seengerema kwa bao 4-2  ambapo mpaka sasa timu zinazochuana kutwaa Ubingwa wa ligi ya mkoa wa Mwanza ni Phantom fc pamoja na Copco veteran ambapo Phantom fc inajumla ya pointi 15 baada ya michezo 6 huku Copco wakiw ana pointi 15 baada ya michezo 6.

IGOMA HEROES YAINYOOSHA ISENI FC LIGI YA MKOA WA MWANZA

Machi 23, 2018
                                                              Timu ya Igoma Heroes

Timu ya soka ya Igoma Heroes ya jijini Mwanza jana ilifanikiwa kuichapa timu ya Iseni fc kwa jumla ya bao 3-2 katika mchezo wa ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Mwanza  mchezo uliopigwa kwenye Uwanja mkongwe wa Nyamagana.

ligi hiyo kwa sasa inaendelea hatua ya 9 bora ambapo timu zinacheza majira ya saa8 mchana na saa 10 jioni  na katika mchezo wa awali Black Mamba iliichapa Vijana fc bao 4-1 katika mchezo wa ligi hiyo.

YANGA MIKONONI MWA MC ALGER KOMBE LA SHIRIKISHO.

Machi 21, 2018
Shirikisho la soka barani Afrika leo limetangaza rasimi ratiba ya kombe la shirikisho katika ratiba hiyo timu ya soka ya Yanga imejikuta ikiangukia mikononi mwa timu ya MC Alger ya nchini Argeria.

mchezo wa awali itafanyika tarehe 7-9 April na marudiano itachezwa aprili 14-16 ifuatayo ni ratiba kamili

Young African (Tanzania) vs MC Alger (Algeria)
TP Mazembe (DR Congo) vs JS kabylie Algeria
AC Leopard (Congo) vs Mbabane swallows (swazland)
FUS Rabat( moroco vs MAS fez (morocco)
Rangers (Nigeria) vs Zesco Utd (zambia)


WANYWAJI WA COCACOLA KANDA YA ZIWA KUJIPATIA TV, PIKIPIKI BUREE

Machi 21, 2018
Kampuni ya Nyanza Bottling Company Limited inayohusika na kutengeneza vinywaji vya Cocacola , Fanta , Sprite na Stone Tangawizi imetangaza neema kwa wakazi wa  kanda ya ziwa kuelekea mashindano ya kombe la Dunia ambalo linatarajia kuanza kutimua vumbi mwezi juni mpaka Julai mwaka huu nchini Urusi ambapo wakazi wa kanda ya ziwa watapata fursa ya kujishindia Soda za Bure, TV- Flat screeen, Fedha za papo kwa papo  pamoja na Bodaboda kwa kununua soda za Cocacola, Fanta aina zote, Sprite pamoja na Stone Tangawizi ambavyo vimekuwa vinywaji vya kukata kiu kwa watanzania .

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mwanza Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Nyanza Bottling Company Limited kwa mikoa ya kanda ya ziwa Samwel Makenge amesema kuwa wameamua kuja na ofa hizo kwa wakazi wa kanda ya ziwa  ili kuongeza msisimko kuelekea kombe la Dunia " sisi kama Kampuni ya Cocacola tumeamua kuwajali wateja wetu ambapo tumeamua kuja na Promosheni ya Cocacola na mzuka wa soka ambapo katika ofa hii wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa watanufaika na ofa hii  kwa kununua soda za Cocacola, Fanta aina zote, Sprite na Stone Tangawizi  ambapo wataweza kujishindia TV Flat screen, Soda za bure, Pesa taslimu pamoja na Bodaboda" alisema

Makenge ameongeza kuwa baada ya mteja  kununua soda ya cocacola na atafunua kizibo kama akikuta  ameshinda ataweza kupata zawadi katika maeneo yafuatayo " kama Mteja wetu akinunua soda na kukuta ameshinda zawadi, zawadi zetu zitatatolewa katika maeneo mbalimbali kwanza kama mteja akishinda zawadi ya soda za bure atapewa zawadi yake dukani aliponunua soda au kwenye gari letu la mauzo, kwa wale watakaoshinda fedha watajipatia fedha Kiwandani au kwa mawakala wetu lakini pia hata kwenye vituo vyetu vilivyoidhinishwa na kampuni yetu, na wale watakaoshinda TV na Pikipiki watapata zawadi zao kiwandani pia na fedha taslimu zitakazotolewa ni kuanzia shilingi 5000, 10000, pamoja na laki moja kwa ujumla fedha ambazo zimetengwa kama zawadi ni shilingi milioni 800" alisema

Makenge amewaomba wakazi wa Kanda ya ziwa kununua vinywaji vya kampuni ya coca-cola kwani wanaweza kujipatia zawadi zilizotajwa " nichukue fursa hii kuwaomba wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kuchangamkia fursa hii kwani wataweza kujipatia zawadi mbalimbali ikiwemo TV ambazo watazitumia kulitazama kombe la Dunia lenyewe kwani tumefanya hivi kwakua sisi Cocacola ndio wadhamini wa kuu wa kombe la Dunia.

JAHAZI LA TOTO AFRICAN LAZIDI KUZAMA

Januari 13, 2018
Timu ya soka ya Toto african ya jijini Mwanza leo imeshindwa kuutumia vyema Uwanja wake wa Nyumbani baada ya kutoka suluhu ya kutofungana na timu ya JKT Oljoro ya mkoani Arusha katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kundi C mchezo uliopigwa leo  Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza
  mchezo huo umechezwa tofauti na ulivyotegemewa ambapo waamuzi katika mchezo huo wamechezesha kwa kiwango cha hali ya juu lakini pia matokeo hayo yanaiweka timu ya Toto african katika hali mbaya zaidi ya kushuka daraja ambapo mpaka sasa imcheza jumla ya michezo 11 na kufanikiwa kujikusanyia pointi 6 pekee .

Matokeo katika ligi hiyo timu ya Biashara fc ya Musoma mkoani Mara  imeichakaza timu ya Alliance kwa bao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Karume Mara huku Dodoma fc wao wakifungwa bao 2-0 na Rinho Rangers mchezo uliopigwa Uwanja wa Alhasan mwinyi Tabora.

PAMBA SC YAINYUKA MUFINDI UNITED NA KUSONGA 32 BORA

Desemba 22, 2017
Timu ya Pamba sc ya jijini Mwanza leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa penati 3-1 baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1 na timu ya Mufindi United katika mchezo wa kombe la FA Cup , mchezo huo Uliopigwa Uwanja wa Wambi Mufindi mkoani Iringa  ulionyeshwa na kituo cha Azam sport HD 2 uliwashuhudia Mufindi United wakiwa wa kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya kwanza ya mchezo lakini dakika mbili kabla ya mapumziko mchezaji wa Pamba sc Seveline Costantine akaifungia Pamba bao la kusawazisha mpaka dakika 90 zinamalizika Pamba sc ikafanikiwa kusonga mbele hatua ya 32 bora ya michuano ya kombe la Azam sports federation baada ya sare ya bao 1-1 penati zikapigwa na Pamba kushinda 3-1.

PAMBA SC YATUA SALAMA IRINGA ,KAMILI KUWAVAA MUFINDI UNITED

Desemba 21, 2017
Klabu ya Pamba sc ya jijini Mwanza tayari imetua salama mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wake wa kombe la FA ambapo inatarajia kucheza na Mufindi United desemba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Wambi wilayani Mufindi mkoani Iringa

Kocha mkuu wa timu hiyo Venance Kazungu ameuambia mtandao huu kwamba timu yake imefika salama " tayari tumefika Iringa na tutawaacha vijana wapumzike na baadae tutajiandaa kuelekea mchezo wetu wa hapo kesho na Mufindi United  " alisema

Mufindi United ya Iringa  iko ligi daraja la kwanza kundi B Tanzania bara ikiwa nafasi ya 6  huku Pamba sports Club pia ikiwa nafasi ya 4 kundi C ikiwa na pointi 12 sawa na Mufindi United.

TOTO AFRICAN YAICHINJA ELEVEN STARS

Desemba 20, 2017
Timu ya soka ya Toto african ya Mwanza leo imefanikiwa kuichapa timu ya Eleven stars  ya Kagera kwa jumla ya bao 2-1 katika mchezo wa kombe la FA uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza baada ya matokeo hayo Toto african imesonga mbele katika hatua zaidi za mashindano hayo.

ITAPENDEZA TOTO AFRICAN IKISHUKA DARAJA?

Desemba 19, 2017


Na Mwandishi wetu , Mwanza

Kwa sasa ligi daraja la kwanza Tanzania bara iko katika mapumziko mafupi ya kupisha dirisha dogo la usajili kwa timu za ligi daraja la pili, daraja la kwanza na ligi kuu bara, wakati ligi hiyo ikiwa katika mapumziko timu ya soka ya Toto African maarufu wanakishamapanda yenyewe iko mkiani mwa ligi hiyo kundi C ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 9 hali ambayo inawafanya wachambuzi wa maswala ya soka kuitabiria timu hiyo huenda ikashuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza kuelekea ligi daraja la pili  kutokana na mwenendo wake katika ligi hiyo ambapo yapo mengi ambayo yanachangia timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika ligi hiyo na kujikuta ikitaka kutengeneza rekodi ya kushuka daraja kutoka ligi kuu, daraja la kwanza na kisha ligi daraja la pili.

VIONGOZI WABABISHAJI
Timu ya soka ya Toto African kwa sasa iko chini ya wanachama wa Yanga wakiongozwa na mtangazaji wa Radio free African Mtani Wambura  ambao walidai kuwa timu  toto ipo katika vipengele vya katiba ya Yanga sasa najiuliza wanakuwaje viongozi wa Toto African wakati sio wanachama wake ? na pia kazi zake za uandishi wa habari na utangazaji zimemshinda? Hakika huu ni ubabaishaji mwingine unaopelekea timu hiyo kuvurunda katika timu hiyo lakini pia hawa yawezekana wametumwa kuisambaratisha timu ya wanakisha mapanda.

KUPOTEZA MECHI KIZEMBE
Wakati ligi daraja la kwanza kundi C ambayo Toto African inashiriki ikiendelea kuliibuka mingong’ono miongoni mwa wadau wa soka jijini Mwanza  kuwa Toto African wameanza kujihusisha na maswala ya kuuza mechi jambo ambalo halijathibitishwa na yeyote mpaka sasa hivyo kama ni kweli hilo nalo linaweza kusababisha timu hiyo kushindwa kuonyesha ushindani wowote katika ligi hiyo kwani yawezekana wachezaji hawapati stahiki zao na kupelekea kutijituma wawapo Uwanjani na tetesi za viashiriavya kuuza mechi vilianzia mechi ya Toto African na Biashara  toto akifungwa bao 3-1 na kisha mechi ya Toto African na Alliance schools ambapo Toto walifungwa bao 4-1.

WACHEZAJI KUTENGWA
Baada ya ligi daraja la kwanza kumalizika kwa mzunguko wa 9 wa ligi hiyo huku timu zikiwa katika mapumziko mafupi na  harakati za kufanya usajili wa dirisha dogo baadhi ya wachezaji wa Toto African ambao waliletwa na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Timu hiyo Wazir Gao kutoka jijini Dar es salaam waligomewa kuhudumiwa huku baadhi ya Viongozi wa Toto wakisema kuwa wachezaji hao waondoke katika timu hiyo kitu ambacho kinaua ukuaji wa soka letu na ustawi wa Toto African kwa ujumla na mpaka sasa wachezaji hao wasiozidi watatu tayari wamesafirishwa kurejea jijini Dar es salaam .

MWENENDO WAKE KATIKA LIGI HIYO
Toto African imekuwa na mwendendo ambao sio mzuri hivyo lazima Uongozi wa juu wa timu hiyo Chini ya mwenyekiti wa timu hiyo Godwin Aiko lazima wajipange upya kuhakikisha kuwa wanaisaidia timu hiyo kufanya vema katika ligi hiyo kwani katika kundi C endapo Toto African wakijiandaa na kufanya usajili katika dirisha dogo wanaweza kujikwamua na kufanya vema lakini endapo wataendeleza mizaha hakika safari ya kushuka daraja itawadia kwao.

MWENYEKITI AITISHA MKUTANO WANACHAMA WAUGOMEA
Novemba 19 mwaka huu  mwenyekiti wa timu ya Toto African Godwin Aiko aliitisha mkutano mkuu wa dharula kwa timu hiyo huku ajenda ikiwa ni kujadili mwenendo wa timu hiyo katika ligi daraja la kwanza ambapo mkutano huo ungefanyika kwenye ukumbi wa bwalo jijini hapa lakini cha ajabu wanachama wa timu hiyo waligoma kujitokeza katika mkutano huo hali ambayo imeendelea kupoteza matumaini ya ushiriki wao katika ligi daraja la kwanza msimu huu lakini siku mbili baadae mkutano ulifanyika na wakaazimia kwa nguvu moja kuungana na kuwa kitu kimoja ili timu hiyo iweze kunusurika kushuka daraja.

USHAURI KWAO
Kutokana na ligi daraja la kwanza kuwa ngumu basi timu hiyo ijipange upya isiweze kushuka daraja kwani ikishuka daraja hakika haitaonekana tena katika medali ya soka.